• Idhaa ya Kiswahili
 • Uchumi
 • Michezo
 • Facebook
 • ChinaABC
 • Sayansi
 • Afya
 • Matukio makubwa yaliyotokea wiki hii (Novemba 5-Novemba 11)

  (GMT+08:00) 2016-11-11 19:21:42

  Umoja wa Mataifa unasema Kuna upungufu mkubwa wa chakula Aleppo

  Umoja wa Mataifa umesema kuwa hifadhi ya chakula ya mwisho imeweza kusambazwa katika eneo linaloshikiliwa na waasi huko Mashariki mwa Aleppo.

  Mratibu wa masuala ya kibinadamu, Jan Egeland, amesema kuwa hakutakua na chakula cha kusambaza wiki ijayo labda umoja wa mataifa wasambaze upya.

  Bwana Egeland ameongeza kuwa Umoja wa Mataifa ulikuwa ametoa mpango wa kina kwa ajili ya kutoa misaada mashariki mwa Aleppo lakini kutokana na masharti ya mara kwa mara imekua vigumu kutoa misaada.

  Umoja wa Mataifa umedai kufanyike usitishwaji wa mapigano zaidi ya saa kumi zilizopendekezwa na Urusi.

  Wakati huo huo Wizara ya Ulinzi ya Urusi imekosoa Umoja wa Mataifa kwa kushindwa kutumia fursa ya kutoa misaada.


  1 2 3 4 5 6 7 8
  Webradio
  Sauti
  6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 1
  12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 2
  20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 3A
  • FM 3B
  Maoni yako