• Idhaa ya Kiswahili
 • Uchumi
 • Michezo
 • Facebook
 • ChinaABC
 • Sayansi
 • Afya
 • Matukio makubwa yaliyotokea wiki hii (Desemba 31-Januari 6)

  (GMT+08:00) 2017-01-06 18:58:05

  Marekani yapeleka wafungwa wa Guantanamo Bay Saudi Arabia

  Kundi la wafungwa wa Yemen waliozuiliwa nchini Marekani katika Gereza la Guantanamo Bay wamewasili nchini Saudi Arabia wiki hii.

  Watu watatu wameonekana wakipokelewa na familia zao katika uwanja wa ndege ambao kwa kawaida hupokea viongozi Mashuhuri mjini Riyadh.

  Kuhamishwa kwa wafungwa kumetokea siku mbili baada ya Ikulu ya Marekani kuahidi kuendelea na mpango wake wa kuhamisha wafungwa kutoka katika Gereza la Guantanamo Bay, wakipinga suala ambalo limekuwa likipingwa vikali na Rais mteule wa Marekani Donald Trump.

  Awali Bw. Donald Trump alikuwa ameitaka serikali ya rais Barack Obama kusitisha uhamishaji wa wafungwa kutoka gereza la kijeshi la Guantanamo huko Cuba.

  Katika ukurasa wake wa Twitter, Bw. Trump amesema, wafungwa wasiachiwe kutoka gereza hilo, kwani watu hao wa hatari hawapaswi kuruhusiwa kurudi tena kwenye medani ya vita.

  Rais Obama ameahidi kufunga gereza hilo katika muda wake na serikali yake imetoa ujumbe kwamba inajaribu kuwahamisha wafungwa wengi zaidi kabla ya rais kuondoka madarakani Januari 20.


  1 2 3 4 5 6 7 8 9
  Webradio
  Sauti
  6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 1
  12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 2
  20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 3A
  • FM 3B
  Maoni yako