• Idhaa ya Kiswahili
 • Uchumi
 • Michezo
 • Facebook
 • ChinaABC
 • Sayansi
 • Afya
 • Matukio makubwa yaliyotokea wiki hii (Desemba 31-Januari 6)

  (GMT+08:00) 2017-01-06 18:58:05

  Kiongozi wa waasi nchini Msumbuji atangaza kurefusha muda wa usitishaji vita

  Kiongozi wa upinzani nchini Msumbuji Afonso Dhlakama ametangaza kurefusha muda wa usimamishaji vita kwa siku 60 baada ya siku saba za mwanzo kumalizika leo.

  Makubaliano ya kusimamisha vita kwa siku saba yalifikishwa wiki iliyopita kati ya rais Filipe Nyusi wa nchi hiyo na Dhlakama.

  Makubaliano hayo mapya yameleta matumaini kuwa wajumbe wa pande zote mbili wanaweza kufikia makubaliano ya amani ya kudumu, na kurejesha uhuru wa wananchi wa Msumbiji kutembea nchini humo bila ya ulinzi wa vikosi vya polisi.

  Mashambulizi pia yatasimamishwa katika miundombinu muhimu ikiwemo njia za reli zinazotumika kusafirisha madini ya shaba kutoka kampuni ya madini ya Vale iliyoko Tete kuelekea bandari za Beira na Nacala.


  1 2 3 4 5 6 7 8 9
  Webradio
  Sauti
  6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 1
  12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 2
  20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 3A
  • FM 3B
  Maoni yako