• Idhaa ya Kiswahili
 • Uchumi
 • Michezo
 • Facebook
 • ChinaABC
 • Sayansi
 • Afya
 • Matukio makubwa yaliyotokea wiki hii (Desemba 31-Januari 6)

  (GMT+08:00) 2017-01-06 18:58:05

  Zaidi ya wafungwa 150 watoroka gerezani Ufilipino

  Zaidi ya wafungwa 150 wametoroka kutoka gerezani baada ya watu kadhaa kushambulia jela moja kusini mwa Ufilipino na polisi bado wanaendelea kuwasaka wafungwa hao.

  Aidha watu hao wenye silaha wamemuua askari jela mmoja na kujeruhi mfungwa mmoja kwenye tukio hilo la Jumanne ambapo ufyatulianaji wa risasi ulidumu kwa karibu saa mbili.

  Maafisa wa magereza wanasema washambuliaji hao walifika saa saba usiku na kuanza kufyatua risasi katika gereza hilo lenye wafungwa zaidi ya 1,500.

  Haijajulikana mara moja ni nani walihusika na uhalifu huo lakini polisi wanashuku kuwa washambuliaji hao wana uhusiano na makundi ya Kiislamu yanayotaka kujitenga.


  1 2 3 4 5 6 7 8 9
  Webradio
  Sauti
  6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 1
  12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 2
  20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 3A
  • FM 3B
  Maoni yako