• Idhaa ya Kiswahili
 • Uchumi
 • Michezo
 • Facebook
 • ChinaABC
 • Sayansi
 • Afya
 • Matukio makubwa yaliyotokea wiki hii (25 Feb- 3 Machi)

  (GMT+08:00) 2017-03-03 19:56:23
  Jeshi la Syria latangaza kukamata mji wa Palmyra nchini humo

  Jeshi la Syria limetangaza kutwaa mji wa Palmyra ulioko katikati ya nchi hiyo baada ya kupambana na kundi la IS na kulisababshia hasara kubwa. Sasa kikosi cha kutegua mabomu kinafanya ukaguzi mjini kote kwa kuondoa mabomu yaliyotegwa barabarani.

  Taarifa iliyotolewa na jeshi hilo inasema ushindi huo ni muhimu kwa ulinzi wa utamaduni na historia ya mji huo mkongwe, pia ni sambamba na ushindi wa jeshi hilo mashariki mwa Aleppo.

  Jeshi hilo limesema litaendelea kupambana na kundi la IS na makundi mengine ya kigaidi ili kurejesha usalama na utulivu nchini humo.

  Mwezi wa Desemba mwaka jana kundi la IS lilishambulia tena mji huo miezi tisa baada ya kupoteza udhibiti wake kwa jeshi la Syria.

  Habari zaidi zinasema hadi sasa zaidi ya watu 26,000 wamekimbia makazi yao kutoka magharibi mwa mji wa Mosul kutokana na mapambano makali ya kuwatimua wapiganaji wa Kundi la IS kutoka ngome yao kuu ya mwisho nchini Iraq.

  Waziri wa uhamiaji wa Iraq Bw Jassim Mohammed al-Jaf amesema wizara yake imewapokea watu hao katika muda wa siku kumi zilizopita kwenye operesheni za kijeshi zilizofanywa magharibi mwa Mosul. Vikosi vimewaondoa na kuwahamishia raia hao kwenye kambi zilizoko katika mji wa Qayyara na Hammam al-Alil pamoja na kusini mwa Mosul, na kuwapatia vyakula na dawa.

  Mwisho mwa mwezi uliopita waziri mkuu wa Iraq Bw Haider al-Abadi alitangaza kuanza kwa operesheni nyingine ya kuliondoa kundi la IS kutoka magharibi mwa Mosul.

  Umoja wa Mataifa umekadiria kuwa watu takriban laki 7.5 hadi 8 bado wanaishi katika maeneo ya magharibi mwa Mosul, idadi ambayo ni changamoto kwa vikosi vya Iraq katika kuingia katika mji huo.


  1 2 3 4 5 6 7
  Webradio
  Sauti
  6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 1
  12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 2
  20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 3A
  • FM 3B
  Maoni yako