• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Matukio makubwa yaliyotokea wiki hii (1 Aprili-7 Aprili)

    (GMT+08:00) 2017-04-07 20:20:56

    Marekani na Urusi zarushiana maneno juu ya shambulizi la Syria

    Cheche za maneno zimerushwa baina ya Nchi ya Marekani na Urusi dhidi ya shambulizi la Syria.

    Hii ni baada ya Marekani kufyatua makombora dhidi ya Syria.

    Mataifa yanayo unga waasi wanaopambana na utawala wa rais wa Syria Bashar al Assad, yameunga mkono shambulio hilo.

    Uturuki binafsi imeunga mkono makombora hayo, huku Saudia Arabia ikimsifu rais Trump kwa ukakamavu wake na Uingereza imejitolea usaidizi kikamilifu.

    Israel imesema ujumbe wa wazi umetumwa unaopaswa kusikika sio tu Damascus lakini pia Iran na Korea kaskazini.

    Kwa upande wake Iran ambayo kama Urusi inaunga mkono serikali ya Syria imeshutumu shambulio hilo.

    Urusi kupitia kwa Msemaji wa rais Putin (Dmitry Peskov) imesema kwamba kando na kukiuka sheria za kimataifa , Washington imesababisha uharibifu mkubwa katika uhusiano na Moscow.

    Wizara ya mambo ya nje imetangaza kusitishwa kwa makubaliano na jeshi la Marekani yalioundwa kuzuia mashambulio ya angani anga ya Syria.


    1 2 3 4 5 6 7 8 9
    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako