• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Matukio makubwa yaliyotokea wiki hii (1 Aprili-7 Aprili)

    (GMT+08:00) 2017-04-07 20:20:56
     

    5.Mazungumzo ya amani ya Kahrtoum yakutanisha viongozi wa AU

    Mpatanishi mkuu wa Umoja wa Afrika Bw. Thabo Mbeki ameanza mikutano kabla ya duru mpya ya mazungumzo ya amani kati ya serikali ya Sudan, kundi la waasi la SPLM la kaskazini na makundi yaenye silaha ya Darfur.

    Bw. Mbeki am amekutana na msaidizi wa rais wa Sudan Bw. Ibrahim Mahmoud Hamid na mkuu wa timu ya mazungumzo ya serikali. Baada ya mkutano huo, Bw. Hamid amesema wamekubaliana kuendelea na juhudi za kundi la upatanishi la Umoja wa Afrika zinazohusiana na kutimiza amani nchini Sudan na kuyaingiza makundi yenye silaha kwenye waraka wa mazungumzo ya kitaifa.

    Bw. Hamid amesisitiza kuwa serikali iko tayari kurejesha mazungumzo na waasi wa kundi la SPLM la kaskazini na makundi yenye silaha ya Darfur.

    Baadaye Bw. Mbeki atakutana na makamu wa kwanza wa rais Bw. Bakri Hassan Saleh, kiongozi wa kundi la upinzani Bw. Al-Sadiq al-Mahdi na kamati ya utekelezaji wa makubaliano ya mazungumzo ya taifa.


    1 2 3 4 5 6 7 8 9
    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako