• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Matukio makubwa yaliyotokea wiki hii (16 Juni-23 Juni)

    (GMT+08:00) 2017-06-23 19:43:37

    5-Nchi za kiarabu zaipatia Qatar masharti

    Nchi nne za muungano wa kiarabu zimeitumia Qatar masharti 13 waizingatie iwapo inataka kuondolewa vikwazo kulingana na vyombo vya habari.

    Saudia, Misri, UAE na Bahrain zinataka taifa hilo kufunga kitu chake cha habari cha Aljazeera.

    Pia wanaitaka Qatar kupunguza ushirikiano na Iran na kufunga kambi moja ya wanajeshi ya Uturuki katika kipindi cha siku 10 pekee.

    Qatar imekana kufadhili magaidi hatua inayosababisha ukosefu wa usalama katika eneo hilo.

    Taifa hilo limekabiliwa na vikwazo vya kidiplomasia na kiuchumi kwa kipindi cha wiki mbili ikiwa ni mgogoro mbaya zaidi wa kisiasa kati ya mataifa hayo ya Ghuba kwa miongo kadhaa.

    Orodha hiyo ilitangazwa baada ya waziri wa maswala ya kigeni nchini Marekani Rex Tillerson kuwaambia majirani wa Qatar ''kuweka mahitaji yao na kuchukua hatua''.

    Waandishi wanasema kuwa Marekani ambayo inataka kutatua mzozo huo imekuwa na matatizo, kuhusu kipindi cha Saudia na mataifa mengine kuweka rasmi mahitaji yao.


    1  2  3  4  5  6  7  
    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako