• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Matukio makubwa yaliyotokea wiki hii (16 Juni-23 Juni)

    (GMT+08:00) 2017-06-23 19:43:37

    6 Korea Kusini yafanya tena jaribio la silaha zake

    Korea kaskazini inadaiwa kutekeleza jaribio jingine la mashine ya kurushia makombora yake .

    Jaribio hilo linadaiwa kutekelezwa siku ya Jumatano wiki hii na litakuwa jaribio la kwanza la mashine kama hiyo kutekelezwa na Korea Kaskazini tangu mwezi Machi.

    Habari hiyo inajiri wakati ambapo kuna wasiwasi kati ya washington na Pyongyang kuhusu mpango wa kinyuklia wa Korea kaskazini.

    Licha ya kukashifiwa ,Korea Kaskazini imeongeza majaribio yake ya makombora kwa lengo la kutengeza kombora linaloweza kurushwa kutoka bara moja hadi jingine.

    Shirika la ujasusi la Marekani limeonya mwezi uliopita kwamba Korea Kaskazini linakaribia kufanikiwa katika mpango huo.

    Maafisa wa Marekani waliokuwa wakizungumza kwa vitengo kadhaa vya habari walisema hatua hiyo ya hivi karibuni siku ya Alhamisi ni awamu ya kwanza ya kutengeza kombora la masafa marefu ambalo litaweza kufika Marekani.


    1  2  3  4  5  6  7  
    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako