• Idhaa ya Kiswahili
 • Uchumi
 • Michezo
 • Facebook
 • ChinaABC
 • Sayansi
 • Afya
 • Matukio makubwa yaliyotokea wiki hii (19 Agosti-25 Agosti)

  (GMT+08:00) 2017-08-25 15:28:59

  Rais Buhari awasili nyumbani baada ya miezi mitatu London

  Rais wa Nigeria Muhammadu Buhari, amewasili nyumbani katika mji mkuu Abuja, baada ya likizo ya matibabu ya miezi mitatu mjini London.

  Wafuasi waliimba na kucheza densi walijipanga kwenye barabara za mji, ambapo maafisa wa ngazi za juu serikalini walikusanyika kumkaribisha Buhari.

  Buhari amefanya safari ya kupata matibabu London mara tatu tangu mwezi Juni mwaka uliopita.

  Pindi tu baada ya kurejea Nigeria rais Buhari,amelazimika kufanya kazi nyumbani kwa wiki tatu baada ya panya kuvamia na kuharibu afisi yake.

  Msemaji wa rais anasema afisi ya Buhari inakarabatiwa baada ya panya kuharibu fanicha na kiyoyozi ndani ya afisi hiyo.

  Aliongeza kuwa huku ikiwa bwana Buhari hawezi kufanya kazi katika afisi yake kutokana na hali ya afisi yake kwa sasa ,hatua yake ya kufanya kazi nyumbani haitaathiri kivyovyote utendakazi wake kwa njia yoyote.


  1  2  3  4  5  6  7  8  
  Webradio
  Sauti
  6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 1
  12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 2
  20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 3A
  • FM 3B
  Maoni yako