• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Matukio makubwa yaliyotokea wiki hii (19 Agosti-25 Agosti)

    (GMT+08:00) 2017-08-25 15:28:59

    Korea Kusini na Marekani zaanza luteka ya pamoja ya mwaka huu

    Majeshi ya Korea Kusini na Marekani yameanza luteka ya pamoja ya mwaka huu.

    Wizara ya ulinzi ya Korea Kusini imesema, luteka hiyo inayoanzia leo hadi mwishow a mwezi huu inalenga kulinda usalama wa Korea Kusini.

    Vyombo vya habari vya Korea Kusini vimesema idadi ya wanajeshi wa Korea Kusini wanaoshiriki kwenye luteka hiyo ni elfu 50, lakini idadi ya wanajeshi wa Marekani ni elfu 17.5, ambayo imepungua kwa elfu 7.5 kuliko mwaka jana.

    Waziri wa ulinzi wa Marekani Bw. James Mattis amesema kupunguza idadi ya wanajeshi wa Marekani ni kwa sababu luteka ya mwaka huu inahusiana zaidi na uongozi na udhibiti wa mapambano.

    Naye msemaji wa wizara ya mambo ya nje ya China bibi Hua Chunying amesema luteka hiyo haisaidii kupunguza mvutano katika peninsula ya Korea, na China inazihimiza pande husika kufikiria pendekezo lake linaloitaka Korea Kaskazini kusimamisha majaribio ya makombora ya nyukilia, na Marekani na Korea Kusini kusimamisha luteka ya kijeshi ya pamoja.

    Pia amesema pande husika zinatakiwa kuchukua hatua zinazosaidia kupunguza mvutano na kurudisha mazungumzo ya amani kuhusu suala la nyuklia la peninsula ya Korea.

    Lakini huku mazoezi hayo ya pamoja yakianza, Korea Kaskazini imetishia kujibu vikali zoezi hilo la pamoja.

    Msemaji wa jeshi kutoka Kaskazini alisema kuwa anatazama kwa makini kile ilichokitaja mchezo wa kivita wa Marekani .

    Pyongyang imetishia kurusha makombora katika bahari ya kisiwa cha Guam ambacho kina kambi kubwa ya wanahewa wa Marekani .


    1  2  3  4  5  6  7  8  
    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako