• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Matukio makubwa yaliyotokea wiki hii (19 Agosti-25 Agosti)

    (GMT+08:00) 2017-08-25 15:28:59

    Vikosi vya Iraq vyakomboa vijiji 12 kaskazini mwa nchi hiyo

    Vikosi vya usalama vya Iraq vinavyopambana na wapiganaji wa kundi la Islamic State vimekomboa vijiji 12 katika siku ya kwanza ya operesheni mpya wiki hii ya kuukomboa mji wa Tal Afar na maeneo ya karibu kutoka kwa kundi hilo.

    Kamanda wa operesheni ya pamoja Luteni Jenerali Abdul-Amri amesema vikosi hivyo na vikundi vya Hashd Shaabi vilizingira vitongoji karibu na mji wa Tal Afar unaodhibitiwa na kundi la IS, kilomita 70 magharibi mwa mji wa Mosul.

    Vikosi hivyo pia vimekomboa barabara kati ya mji wa Tal Afar na wilaya ya Mahalabiyah, na kukata njia ya ugavi kati ya sehemu mbili zinazodhibitiwa na IS.

    Habari nyingine zimesema Umoja wa Mataifa siku hiyo ulionya kuwa maelfu ya wairaq wanatarajiwa kukimbia mji wa Tal Afar na maeneo ya jirani, baada ya vikosi vya usalama vya nchi hiyo kuanza operesheni ya kukomboa sehemu hizo jimboni Nineveh.


    1  2  3  4  5  6  7  8  
    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako