• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Matukio makubwa yaliyotokea wiki hii (14 Oktoba-20 Oktoba)

    (GMT+08:00) 2017-10-20 17:27:55

    Mkutano wa 18 wa chama cha CPC wafanyika

    Mkutano mkuu wa 19 wa Chama cha Kikomunisti cha China ulifunguliwa Alhamisi mmjini Beijing. Kwa niaba ya kamati kuu ya 18 ya chama hicho, Bw. Xi Jinping amehutubia mkutano huo akitangaza kuwa, kwa kufuata itikadi ya Ujamaa wenye umaalumu wa China katika kipindi kipya, Chama cha Kikomunisti cha China kitaongoza wananchi wa China kukamilisha kazi ya kujenga jamii yenye maisha bora kwa pande zote.

    Katika miaka 5 iliyopita, Chama cha Kikomunisti cha China kimeimarisha uongozi wake, na kutekeleza mawazo na mikakati mingi mipya ya utawala. Hivi sasa China inachangia asilimia 30 ya ongezeko la uchumi wa dunia, na kufanikiwa kuwasaidia watu zaidi ya milioni 60 kuondokana na umaskini. Bw. Xi amesema maendeleo ya China yamefungua ukurasa mpya wa kihistoria.

    Mkutano mkuu wa 12 wa Chama cha Kikomunisti cha China uliofanyika zaidi ya miaka 30 iliyopita ulitoa uamuzi wa kujenga Ujamaa wenye umaalumu wa China kwa mara ya kwanza, na Ujamaa wenye umaalumu wa China ulianza kuwa kiini cha nadharia na majaribio ya utawala wa chama baada ya utekelezaji wa sera ya mageuzi na ufunguaji mlango.

    Rais Xi alisema mkutano huu wa 19 umerithi nia ya awali, na pia kuiendeleza na kufanya uvumbuzi, kwa kutangaza Ujamaa wenye umaalumu wa China umeingia katika kipindi kipya.


    1  2  3  4  5  6  7  
    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako