• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Matukio makubwa yaliyotokea wiki hii (14 Oktoba-20 Oktoba)

    (GMT+08:00) 2017-10-20 17:27:55

    Kamishena wa tume ya uchaguzi Kenya ajiuzulu

    Mmoja wa maafisa wakuu wa Tume ya Uchaguzi Kenya (IEBC) Dkt. Roselyn Akombe ametangaza kujiuzulu katika tume hiyo chini ya wiki moja kabla ya uchaguzi mpya wa urais kufanyika nchini humo.

    Ametangaza kwamba anahofia usalama wake na hatarajii kurejea Kenya hivi karibuni.

    Dkt Akombe ametuma taarifa kutoka mjini New York anakoishi ambapo alikuwa akiufanyia kazi Umoja wa Mataifa kabla ya kujiunga na tume ya IEBC.

    Katika taarifa, Dkt Akombe alisema kuwa merejeleo ya uchaguzi utakaofanyika hayaafikii matarajio ya uchaguzi ulio huru na wa haki.

    Tume ya IEBC imesema imesikitishwa na hatua ya Dkt Akombe kujiuzulu na kuahidi kutoa taarifa ya kina baadaye.

    Wakati huo huo Kiongozi wa muungano wa upinzani nchini Kenya Raila Odinga ameitisha maandamano ya nchi nzima tarehe 26, siku ambayo Uchaguzi mpya wa urais umepangwa kufanyika.

    Raila Odinga ambaye alijitoa katika Uchaguzi huo amesisitiza kuwa Uchaguzi hauwezi kufanyika bila mabadiliko ndani ya Tume ya Uchaguzi.

    Mwenyekiti wa Tume hiyo ya Uchaguzi Wafula Chebukati tayari amesema kuwa anatilia shaka, iwapo uchaguzi huo utakuwa huru na haki iwapo viongozi wa kisiasa nchini humo hawatazungumza na kutatua mzozo wa kisiasa unaoendelea.


    1  2  3  4  5  6  7  
    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako