• Idhaa ya Kiswahili
 • Uchumi
 • Michezo
 • Facebook
 • ChinaABC
 • Sayansi
 • Afya
 • Matukio makubwa yaliyotokea wiki hii (Februari 3-Februari 9)

  (GMT+08:00) 2018-02-09 17:54:15

  Gambia yajiunga tena na Jumuiya ya Madlola

  Takriban miaka mitano baada ya kujitoa katika jumuiya ya madola leo Gambia inajiunga upya.

  Alhamisi wiki hii Sherehe imefanyika katika makao makuu ya jumuiya hiyo mjini London kuidhinisha kurudi kwa nchi hiyo kama taifa mwanachama wa jumuiya ya madola.

  Mnamo Februari 2017, rais mpya aliyechaguliwa Adama Barrow aliomba nafasi ya taifa lake kurudi kuwa mwanachama, na mwezi Desemba bunge nchini humo liliidhinisha ombi hilo la kurudi katika kundi hilo linalojumuisha mataifa yaliokuwa chini ya ukoloni wa Uingereza.

  Gambia ilijiondoa katika jumuiya hiyo mnamo Octoba 2013 wakati wa utawala wa rais Yahya Jammeh.

  Yahya Jammeh aliishutumu Uingereza kwa kuwaunga mkono wapinzani wake wa kisiasa.

  Baada ya Afrika kusini, Pakistan na Fiji, sasa Gambia inakuwa nchi ya nne kurudi katika jumuiya ya madola.

  Afrika kusini ilitangaza kujitoa katika jumuiya hiyo mnamo Mei mwaka 1961 baada ya kupitisha sheria ilioifanya nchi hiyo kuwa Jamhuri na kusitisha utawala wa malkia.

  Ilijunga upya miaka 33 baadaye mnamo 1994 baada ya kumalizika kwa ubaguzi wa rangi nchini.


  1  2  3  4  5  6  7  8  
  Webradio
  Sauti
  6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 1
  12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 2
  20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 3A
  • FM 3B
  Maoni yako