• Idhaa ya Kiswahili
 • Uchumi
 • Michezo
 • Facebook
 • ChinaABC
 • Sayansi
 • Afya
 • Matukio makubwa yaliyotokea wiki hii (Februari 3-Februari 9)

  (GMT+08:00) 2018-02-09 17:54:15

  Mwanasiasa wa upinzani Kenya afurushwa na kupelekwa Canada.

  Mwanasiasa wa muungano wa upinzani nchini Kenya Nasa, Miguna Miguna amefurushwa na kupelekwa nchini Canada.

  Miguna alikamatwa Ijumaa iliopita kwa kuhusuka na uapishaji wa kiongozi wa upinzani nchini humo Raila Odinga, na jaji wa mahakama kuu James Wakiaga akimwachilia kwa dhamana ya dola 500 lakini hakuachiliwa.

  Mawakili wake Nelson Havi na Cliff Ombeta wamesema kuwa waliarifiwa kwamba bwana Miguna aliingizwa katika ndege iliokuwa ikielekea Amsterdam na baadaye kuelekea Canada.

  Serikali kupitia kwa mkuuu wa sheria ilikuwa imeonywa kwamba kujiapisha kwa Odinga ni kosa la uahini ambalo adhabu yake ni kifo.

  Wizara ya mambo ya ndani nchini humo imesema Miguna Miguna alipata hati ya kusafiria ya Kenya kinyume cha sheria na hivyo kutimuliwa kwake kwenda nchini Canada hakukukiuka sheria za nchi wala haki zake.

  Katika taarifa ya wizara ya mambo ya ndani ya Kenya msemaji wa wizara hiyo Mwenda Njoka amesema bwana Miguna "kwa makusudi alishindwa" kuweka wazi kuwa alikuwa na uraia wan chi nyingine wakati alipopatiwa hati ya kusafiria ya Kenya mnamo Machi 2009.


  1  2  3  4  5  6  7  8  
  Webradio
  Sauti
  6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 1
  12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 2
  20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 3A
  • FM 3B
  Maoni yako