• Idhaa ya Kiswahili
 • Uchumi
 • Michezo
 • Facebook
 • ChinaABC
 • Sayansi
 • Afya
 • Matukio makubwa yaliyotokea wiki hii (Februari 3-Februari 9)

  (GMT+08:00) 2018-02-09 17:54:15

  Burundi yaishutumu UNHCR kwa kughushi takwimu za wakimbizi

  Serikali ya Burundi wiki hii imelishutumu Shirika la Kuhudumia Wakimbizi la Umoja wa Mataifa UNHCR kwa kughushi takwimu za wakimbizi wa nchi hiyo.

  Akizungumzia ombi la UNHCR la kuongezewa fedha zaidi kwa ajili ya kuwasaidia wakimbizi wa Burundi kwa mwaka huu, msaidizi wa waziri wa mambo ya ndani wa nchi hiyo Bw. Therence Ntahiraja amesema, Shirika hilo halijakubali kuwa baadhi ya wakimbizi wamerejea makwao, bali imeongeza idadi ya wakimbizi kwa lengo la kupata kazi.

  Jumanne wiki hii, UNHCR ilitoa taarifa ikisema inahitaji dola milioni 391 za kimarekani kwa ajili ya kuwahudumia wakimbizi zaidi ya laki 4 wa Burundi mwaka huu, na kwamba fedha zaidi zinahitajika ili kuzuia mgogoro huo kusahaulika.

  Pia limesema kuwa idadi ya wakimbizi inatarajiwa kuongezeka kwa zaidi ya elfu 50 mwaka huu kwa kuwa juhudi za kikanda za kusuluhisha mgogoro wa kisiasa nchini humo hazijapata mafanikio makubwa.


  1  2  3  4  5  6  7  8  
  Webradio
  Sauti
  6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 1
  12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 2
  20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 3A
  • FM 3B
  Maoni yako