• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Matukio makubwa yaliyotokea wiki hii (Februari 3-Februari 9)

    (GMT+08:00) 2018-02-09 17:54:15

    Rais wa Maldives atangazwa siku 15 za hali ya hatari huku Rais wa zamani akikamatwa

    Rais wa zamani wa Maldives Maumoon Abdul Gayoom mapema jumanne hii amekamatwa na kikosi maalum cha polisi, saa chache baada ya Rais Abdulla Yameen kutangaza hali ya hatari ya siku 15.

    Gayoom alikamatwa akiwa nyumbani kwake kwenye mji mkuu wa taifa hilo akiwa na mwanaye wa kiume ambaye pia alikamatwa. Wawili hao wanatuhumiwa kupanga njama ya kupindua serikali.

    Katika ujumbe wake wa twitter, Gayoom amesema kukamatwa kwake ni kinyume cha sheria.

    Jumatatu Rais wa Maldives, kupitia Waziri wa Sheria alitangaza siku 15 za hali ya hatari, ambapo hata hivyo amewahakikishia usalama raia wa Maldives pamoja na jamii za wageni waliotembelea ama wale wanaoishi nchini humo.

    Lakini pamoja na usalama huo kuna baadhi ya haki zitazuiliwa, huku shughuli za kiutalii, usafiri wa anga na biashara ikitangazwa kuwa havitaguswa.

    Wakati huo huo Katibu mkuu wa Umoja wa Mataifa Bw. António Guterres, ameitaka serikali ya nchi hiyo kufuta hali ya dharura iliyotangazwa haraka iwezekanavyo.

    Bw. Guterres ameitaka serikali ya Maldives kuheshimu katiba na kutawala nchi kwa mujibu wa sheria, na kuwahakikishia usalama wa watu wote wakiwemo maofisa wa mahakama.


    1  2  3  4  5  6  7  8  
    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako