• Idhaa ya Kiswahili
 • Uchumi
 • Michezo
 • Facebook
 • ChinaABC
 • Sayansi
 • Afya
 • Matukio makubwa yaliyotokea wiki hii (March 10-March 16)

  (GMT+08:00) 2018-03-16 20:20:17

  Watu 12 wafariki Ajali ya helikopta Senegal

  Watu wanane wameuawa na 12 kujeruhiwa nchini Senegal baada ya helikopta ya kijeshi kuanguka nchini Senegal.

  Ripoti zinasema kuwa ajali hiyo imetokea katika eneo la Missirah, katika mpaka wa Kaskazini karibu na nchi ya Gambia.

  Helikopta hiyo ilikuwa inawasafirisha watu 20 waliokuwa wanarejea nyumbani baada ya kuhudhuria mazishi katika eneo la Ziguinchor, Kusini mwa jiji kuu Dakar.

  Rais Macky Sall, ametuma risala za rambirambi kwa jamaa ndugu na marafiki wa watu waliopoteza maisha na kuagiza uchunguzi kufanyika kubaini kilichosababisha ajali hiyo.

  Mara ya mwisho kutokea kwa ajali ya ndege nchini Senegal ilikuwa ni mwaka 2015, wakati abiria saba walipopoteza maisha baada ya kupata ajali.

  1  2  3  4  5  6  7  8  
  Webradio
  Sauti
  6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 1
  12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 2
  20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 3A
  • FM 3B
  Maoni yako