• Idhaa ya Kiswahili
 • Uchumi
 • Michezo
 • Facebook
 • ChinaABC
 • Sayansi
 • Afya
 • Matukio makubwa yaliyotokea wiki hii (March 10-March 16)

  (GMT+08:00) 2018-03-16 20:20:17

  Rais wa Mauritius akataa kujiuzulu kwa madai ya ufisadi

  Rais wa Mauritius Ameenah Gurib-Fakim amekataa kujiuzulu licha ya tuhma za kutumia fedha za taasisi inayoshughulikia masuala ya Sayansi lenye mako yake jijini London nchini Uingereza Planet Earth Institute (PEI) kununua mavazi na vitu vingine vya kibinafsi.

  Gurib-Fakim, rais pekee mwanamke barani Afrika, ametuhumiwa kuchukua Dola 26,000 makusudi kutoka kwenye akaunti ya taasisi hiyo kwa matumizi binafsi.

  Wiki iliyopita, Waziri Mkuu Pravind Jugnauth alitangaza kuwa rais huyo alikuwa amekubali kujiuzulu siku ya Jumatatu, siku ambayo nchi hiyo ilikuwa inaadhimisha miaka 50 ya uhuru wake.

  Hata hivyo, rais huyo amesema madai hayo ni ya uongo na atahakikisha kuwa anasafisha jina lake, na hatajiuzulu.

  Taarifa kutoka Ikulu ilisema kuwa "Mheshimiwa rais Ameenah Gurib-Fakim, hajafanya kosa lolote, hakuna ushahidi dhidi yake na hivyo anakataa shinikizo za kumtaka ajiuzulu,"

  Hata hivyo, taarifa zinasema kuwa rais huyo alichukua fedha hizo kimakosa na tayari zimerejeshwa.

  1  2  3  4  5  6  7  8  
  Webradio
  Sauti
  6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 1
  12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 2
  20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 3A
  • FM 3B
  Maoni yako