• Idhaa ya Kiswahili
 • Uchumi
 • Michezo
 • Facebook
 • ChinaABC
 • Sayansi
 • Afya
 • Matukio makubwa yaliyotokea wiki hii (March 10-March 16)

  (GMT+08:00) 2018-03-16 20:20:17

  Zaidi ya watu elfu 39 wapoteza makazi yao kusini mwa Ethiopia

  Jeshi la Ethiopia limesema vurugu zilizotokea katika eneo la Moyale kusini mwa nchi hiyo limesababisha watu zaidi ya elfu 39 kupoteza makazi.

  Ofisa mwandamizi wa jeshi Kanali Aligaz Gebre, amesema uvumi kuhusu uwezekano wa kutoka kwa vita ndio umefanya watu hao kukimbia makazi yao. Bw. Gabre amesema hayo siku chache baada ya kuvunjika kwa operesheni ya kuwatoa waasi katika eneo la Moyake iliyosababisha watu 9 kuuawa na wengine 12 kujeruhiwa.

  Matukio ya kufyatuliana risasi na mkanganyiko vimefanya watu zaidi ya elfu 8 kukimbilia nchi jirani ya Kenya.

  Mji wa Moyale ulioko kwenye Jimbo la Oromia kusini mwa Ethiopia karibu Kenya, limekuwa katika hali ya vurugu tangu mwaka 2015, mamia ya watu wameuawa na maelfu wamefungwa kutokana na vurugu hizo.

  Kamati ya msalaba mwekundu ya Kenya imetoa taarifa ikisema hadi sasa idadi ya wakimbizi wa Ethiopia waliokimbilia nchini Kenya imefikia 8,592 tangu tarehe 10 mwezi huu, na idadi hiyo inatarajiwa kuongezeka.

  Taarifa imesema kamati ya msalaba mwekundu ya Kenya imewapatia wakimbizi hao chakula na huduma za afya, na wamepewa hifadhi katika wilaya ya Moyale ya kaunti ya Marsabit na eneo la Sololo karibu na mpaka wa nchi hizo mbili, kaskazini mwa Kenya. Kazi ya kuandikisha wakimbizi inaendelea.

  1  2  3  4  5  6  7  8  
  Webradio
  Sauti
  6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 1
  12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 2
  20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 3A
  • FM 3B
  Maoni yako