• Idhaa ya Kiswahili
 • Uchumi
 • Michezo
 • Facebook
 • ChinaABC
 • Sayansi
 • Afya
 • Matukio makubwa yaliyotokea wiki hii (March 31-Aprili 6)

  (GMT+08:00) 2018-04-06 20:02:35

  Rais Ian Khama wa Botswana ajiuzulu

  Rais Ian Khama wa Botswana amejiuzulu baada ya kuitumikia nchi yake kwa mihula miwili ya kikatiba, kwa jumla ya miaka 10.

  Khama amekwishakamilisha ziara ya majimbo yote 57 ya Botswana tangu mwezi Desembea, akiwaaga wananchi wake wapatao milioni 2.2.

  Nafasi yake Ikulu inachukuliwa na Makamu wa Rais Mokgweetsi Masisi, ikiwa ni miezi 18 kamili kabla ya kufanyika uchaguzi mkuu nchini humo.

  Katika uongozi wake, Khama anatajwa kufanikisha maendeleo nchini mwake kupitia rasimali ya almasi nchini humo na uuzaji nje nyama, sambamba na kuimarisha utawala bora.

  Anakumbukwa kwa kuwa muwazi— amepata kuvunja itifaki za kidiplomasia wakati fulani kwa kumkosoa waziwazi Rais wa sasa wa Marekani Donald Trump, na pia Rais wa zamani wa Zimbabwe, Robert Mugabe, Zimbabwe ni nchi jirani na Botswana.

  Khama mwenye umri wa miaka 65, amejitengeneza zaidi mwenyewe kiuongozi kuliko ilivyotarajiwa kwamba angebebwa zaidi na jina la baba yake, mzee Seretse Khama aliyeongoza taifa hilo kuanzia mwaka 1966 hadi 1980 akiwa Rais wa kwanza wa Botswana baada ya uhuru kutoka Uingereza.


  1  2  3  4  5  6  7  8  
  Webradio
  Sauti
  6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 1
  12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 2
  20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 3A
  • FM 3B
  Maoni yako