• Idhaa ya Kiswahili
 • Uchumi
 • Michezo
 • Facebook
 • ChinaABC
 • Sayansi
 • Afya
 • Matukio makubwa yaliyotokea wiki hii (Aprili 21-Aprili 27)

  (GMT+08:00) 2018-04-27 19:13:14
  Maandamano mapya yaibuka Madagascar

  Wafuasi 2,000 wa upinzani nchini Madagascar wameingia mitaani Jumatano wiki hii kama mwanzo wa maandamano makubwa yaliyoitishwa na upinzani dhidi ya serikali ya nchi hiyo.

  Wafuasi wa upinzani wamekua wakiandamana kuelekea makao makuu ya Mahakama ya Katiba katika mji mkuu Antananarivo, kuwasilisha ombi la kujiuzulu kwa Rais Hery Rajaonarimampianina.

  Waandamanaji walikusanyika kwenye eneo la Mei 13, huku wakipiga kelelea na kusema "Rajao jiuzulu mara moja.

  Lakini Rais Hery Rajaonairmampianina wa Madagascar amesema maandamano yaliyoongozwa na wapinzani yaliyofanyika jumamosi mjini Antananarivo yalikuwa ni jaribio la mapinduzi.

  Akihutubia taifa jana Rais Rajaonarimampianina amesema Madagascar ni nchi inayoheshimu demokrasia, lakini kilichotokea jumamosi ni jaribio halisi la mapinduzi.

  Ikiwa imesalia miezi saba kabla ya duru ya kwanza ya uchaguzi mkuu, upinzani umekua ukiingia mitaani katika mji mkuu wa nchi hiyo kwa muda wa siku tano mfululizo wakipinga sheria mpya za uchaguzi, ambazo wanadai kwamba zimegemea upande wa serikali pekee.

  Jumanne wiki hii, wabunge wa upinzani waliomba rais Rajaonarimampiania kujiuzulu, wakimshtumu kutaka kuwazuia wapinzani wake.


  1  2  3  4  5  6  7  
  Webradio
  Sauti
  6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 1
  12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 2
  20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 3A
  • FM 3B
  Maoni yako