• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Matukio makubwa yaliyotokea wiki hii (Aprili 21-Aprili 27)

    (GMT+08:00) 2018-04-27 19:13:14

    Zaidi ya watu 15 wauawa kwenye shambulizi kanisani Nigeria

    Mapadri wawili wa kanisa Katoliki na waumini 16 wa kanisa hilo waliuawa katika shambulizi lililotokea katika kijiji cha Mbalom katika jimbo la Benue, nchini Nigeria.

    Shambulizi hilo lililotokea katikati mwa nchi ambako kumeendelea kushuhudiwa mapigano ya kikabila limehusishwa wafugaji waliokua waibebelea silaha.

    Mashahidi wanasema shambulizi hilo lilitokea mapena Jumanne asubuhi Aprili 24.

    Washambuliaji hao waliingia katika kanisa wakati wa sherehe ya mazishi katika kijiji cha Mbalom, katika jimbo la Benue, nchini Nigeria. Mapadri wawili na waumini 16 wa kanisa Katoliki, wote waliuawa kwa kupigwa risasi, kwa mujibu wa mashahidi walionukuliwa na shirika la habari la AFP ambao pia wamesema watu wengi walijeruhiwa.

    Washambuliaji pia walipora katika zaidi ya nyumba 60 na katika maduka ya chakula. Wakazi walikimbilia katika viijiji jirani kwa kuhofia usalama wao.

    Dayosisi ya Makurdi, mji mkuu wa Jimbo la Benue, imelaani vurugu ambazo zilikumba mojawapo ya makanisa yake. Rais Muhammadu Buhari ameahadi kwamba wahalifu wataadhibiwa kwa mujibu wa sheria kwa kutekeleza shambulizi lenye lengo la kuchochea uhasama wa kidini.


    1  2  3  4  5  6  7  
    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako