• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Matukio makubwa yaliyotokea wiki hii (Aprili 21-Aprili 27)

    (GMT+08:00) 2018-04-27 19:13:14

    Chama tawala cha Zambia chakaribisha ushindi kwenye uchaguzi wa serikali za mitaa

    Chama tawala cha Zambia kimesema mafanikio yaliyopatikana kwenye uchaguzi mdogo wa serikali za mitaa yameonyesha kuwa wananchi wa Zambia hawakubali vyama vya upinzani.

    Chama tawala cha Patriotic Front cha Zambia kimepata viti vyote saba kwenye ngome zake, na pia kimechukua viti vitano kati ya tisa ambavyo hapo awali vilishikiliwa na chama kikuu cha upinzani cha UPND, na kiti kimoja kati ya hivyo ambacho kina mgogoro kunasubiri uamuzi wa tume ya uchaguzi ya Zambia, ambayo imefanya chaguzi ndogo 16 za serikali za mikoa tarehe 24 mwezi huu.

    Katibu mkuu wa chama tawala cha Zambia Bw Davies Mwila amewaambia wanahabari kuwa matokeo ya uchaguzi huo yameashiria kuwa chama tawala bado kina nguvu.

    Na huku hayo yakijiri nayo nchi jirani ya Zimbabwe inajiandaa kwa uchaguzi Mkuu uliopangwa kufanyika mwezi Julai.

    Utakuwa ni Uchaguzi wa kwanza bila ya rais wa zamani wa nchi hiyo Robert Mugabe aliyetimuliwa madarakani mwaka uliopita.

    Rais wa Zimbabwe Emmerson Mnangagwa alitangaza kwamba Uchaguzi Mkuu uliopangwa kufanyika mwaka huu nchini Zimbabwe unapaswa kufanyika kabla ya mwezi Julai.


    1  2  3  4  5  6  7  
    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako