• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Matukio makubwa yaliyotokea wiki hii (Aprili 21-Aprili 27)

    (GMT+08:00) 2018-04-27 19:13:14

    Ramaphosa asitisha ziara machafuko yakigubika Magharibi mwa nchi

    Rais wa Afrika Kusini Cyril Ramaphosa amelazimika kusitisha ziara yake nchini Uingereza kuhudhuria mkutano wa viongozi kutoka mataifa ya Jumuiya ya Madola ili kurejea nyumbani kutokana na machafuko yanayoshuhudiwa Kaskazini Magharibi mwa nchi hiyo.

    Wakaazi wa mkoa huo wamekuwa wakiandamana, na kupora mali za wafanyibiashara hasa kutoka nje ya nchi hiyo kwa madai ya kuwa wanataka ajira, makaazi bora na kumalizwa kwa ufisadi.

    Shughuli zimekwama katika mji mkuu wa mkoa wa Mahikeng, huku maduka yakisalia kufungwa na waandamanaji kuteketeza kwa moto matairi barabarani wakitaka pia kujiuzulu kwa viongozi wa mkoa huo.

    Rais Ramaphosa anarejea nyumbani kujaribu kumaliza machafuko hayo ambayo yameelezwa na kiongozi wa eneo hilo Supra Mahumapelo kuwa yamechochewa kisiasa.

    Kuporwa kwa mali na uharibu unatokea ni pigo kwa serikali ya rais Ramaphosa ambaye wiki hii, ametumia muda mwingi akiwa jijini London kuwashawishi wawekezaji kuja kuwekeza nchini humo.

    Rais Ramaphosa ametaka kuwepo kwa utulivu na kutoa wito kwa polisi kutotumia nguvu kupitia kisiasa dhidi ya waandamanaji.


    1  2  3  4  5  6  7  
    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako