• Idhaa ya Kiswahili
 • Uchumi
 • Michezo
 • Facebook
 • ChinaABC
 • Sayansi
 • Afya
 • Matukio makubwa yaliyotokea wiki hii (Juni 23-Juni 29)

  (GMT+08:00) 2018-06-29 18:47:12

  Watu watano wameuawa na wengine kadhaa wamejeruhiwa katika tukio la ufyatuaji risasi Marekani

  Watu watano wameuawa na wengine kadhaa wamejeruhiwa vibaya kwenye tukio la ufyatuaji risasi dhidi ya umati wa watu, lililotokea katika jengo la ofisi za gazeti moja mjini Annapolis, katika jimbo la Maryland nchini Marekani.

  Polisi wamesema muuaji alitumia gobole na alifanya uhalifu huo peke yake. Polisi wamemkamata mtu huyo na sasa wanamhoji. Msemaji wa ofisi ambayo tukio hilo limetokea, baada ya kufyatua risasi kadhaa, muuaji huyu aliacha ghafla kufyatua risasi.

  Tukio hilo lilitokea usiku wa manane, na polisi walifika kwenye eneo la tukio haraka, na watu waliokuwa kwenye jengo walionekana wakitoka wakiweka mikono kichwani.

  Rais Donald Trump wa Marekani amearifiwa kuhusu tukio hilo, na kuwapa pole wahanga na familia za walioathiriwa na tukio hilo.


  1  2  3  4  5  6  7  8  
  Webradio
  Sauti
  6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 1
  12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 2
  20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 3A
  • FM 3B
  Maoni yako