• Idhaa ya Kiswahili
 • Uchumi
 • Michezo
 • Facebook
 • ChinaABC
 • Sayansi
 • Afya
 • Matukio makubwa yaliyotokea wiki hii (Juni 23-Juni 29)

  (GMT+08:00) 2018-06-29 18:47:12

  Rais Recep Tayyip Erdogan ashinda Urais Uturuki

  Tume ya uchaguzi nchini Uturuki imemtangaza Rais Recep Tayyip Erdogan kama mshindi wa nafasi ya urais katika uchaguzi mkuu uliofanyika June 24.

  Erdogan ambaye aliingia madarakani 2014 ameshinda muhula wake wa pili kwa asilimia 53 ya kura zote zilizohesabiwa akiepuka kuingia mzunguko wa pili huku chama chake kikishinda wingi wa viti bungeni.

  Mpinzani wake mkuu Muharrem Ince kutoka chama cha CHP tayari amempongeza Erdogan katika mitandao ya kijamii licha ya kushutumu uchaguzi huo kuwa haukuwa wa haki.

  Muda mfupi kabla ya kura halisi kutangazwa Erdogan alizungumza kupitia televishen ya taifa akisema taifa lake limepata taarifa nzuri za yeye kuendelea kusalia madarakani licha ya kwamba hazikua bado za uhakika.

  Erdogan ambaye alihutubia mamia ya wafuasi wake mjini Ankara, kwa sasa atapata mamlaka makubwa zaidi chini ya katiba ya nchi hiyo ambayo itaanza kutumika baada ya uchaguzi.

  Baadhi ya wakosoaji wanasema kuwa jambo hilo litashuhudia nguvu nyingi atakazokuwa nazo mtu mmoja, na kwamba Uturuki imeshindwa kuona namna maafisa wengine wa serikali wanavyopaswa wakitolea mfano kwa Ufaransa na Marekani.

  Tume ya uchaguzi imesema Chama cha kikurdi nacho kimefanikiwa kupata asilimia 10%.

  Kulikuwa na wagombea wengine wanne katika uchaguzi wa urais, na hakuna hata mmoja ambaye anaonekana kuwa amepata ushindi mkubwa.


  1  2  3  4  5  6  7  8  
  Webradio
  Sauti
  6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 1
  12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 2
  20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 3A
  • FM 3B
  Maoni yako