• Idhaa ya Kiswahili
 • Uchumi
 • Michezo
 • Facebook
 • ChinaABC
 • Sayansi
 • Afya
 • Matukio makubwa yaliyotokea wiki hii (Juni 23-Juni 29)

  (GMT+08:00) 2018-06-29 18:47:12

  Rais wa Syria asema uingiliaji kutoka nchi za nje umesababisha vita nchini Syria

  Rais Bassar al-Asad wa Syria amesema wiki hii kwamba, sababu muhimu ya vita vilivyodumu kwa miaka mingi nchini Syria ni nchi za kigeni ikiwemo Marekani kuunga mkono makundi ya upinzani, hasa kuingilia kati ya mambo ya ndani ya Syria kwa njia ya kijeshi.

  Amesema serikali yake itafanya juhudi kuhimiza maafikiano ya pande zote, lakini kama magaidi hawatajisalimisha, serikali itaendelea kupambana nao.

  Hivi sasa nchi kadhaa za Magharibi zinayapanga upya makundi yenye msimamo mkali ili kuyarudisha nchini Syria katika siku za baadaye.

  Habari nyingine zinasema, ndege 11 za jeshi la Russia hivi karibuni zimerudi nchini humo kutokea Syria, na askari kadhaa kwenye kituo cha jeshi la anga cha Russia huko Hmeymim nchini Syria pia watarejea nchini mwao baada ya kumaliza majukumu yao.

  Wakati huo huo wiki hii Jeshi la Syria limetwaa tena maeneo ya kilomita za mraba 1,800 kutoka kwa kundi la Islamic State mashariki mwa Syria karibu na mpaka wa Iraq.

  Taarifa iliyotolewa na jeshi hilo inasema jeshi la Syria na washirika wake wametekeleza operesheni sahihi dhidi ya maeneo yaliyodhibitiwa na IS mashariki mwa mkoa wa Deir al-Zour, ikiwa ni sehemu ya operesheni kubwa ya jeshi hilo kwenye eneo la jangwa mashariki mwa Syria, ambako jeshi hilo limeteka maeneo makubwa katika siku za karibuni.


  1  2  3  4  5  6  7  8  
  Webradio
  Sauti
  6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 1
  12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 2
  20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 3A
  • FM 3B
  Maoni yako