• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Matukio makubwa yaliyotokea wiki hii (Juni 23-Juni 29)

    (GMT+08:00) 2018-06-29 18:47:12

    Umoja wa Ulaya wakubaliana masuala ya wahamiaji

    hatimaye viongozi wa Umoja wa Ulaya waliokutana huko Brussels wameafikiana kuhusu masuala ya wahamiaji na hivyo kuepukana na mgogoro mpya.

    Italia imekua imezuia tangu Alhamisi jioni wiki hii kupitishwa kwa maazimio ya pamoja katika mkutano wa Umoja wa Ulaya wa Brussels, kwa kuomba nchi nyingine kujibu kwanza madai yake kuhusu suala la wahamiaji, hali ambayo ilitaka kuzua mgawanyiko mkubwa ndani ya Umoja wa Ulaya.

    Nchi hizo ishirini na nane za Umoja wa Ulaya pia zimeamua kuidhibiti mipaka yao ya nje, hasa kwa kuiongezea misaada Uturuki na Afrika Kaskazini, ili kuepuka kurudi kwa wimbi la wahamiaji na wakimbizi sawa na lile lililoshuhudiwa Ulaya mnamo mwaka 2015.

    Rais wa serikali ya Italia Giuseppe Conte, amekaribisha matokeo ya mkutano huo na kusema kuwa Italia haiko "peke yake". Roma itaamua baadaye ikiwa ni lazima au la kuwa na vituo vya mapokezi kwa wahamiaji, ameongeza.


    1  2  3  4  5  6  7  8  
    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako