• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Matukio makubwa yaliyotokea wiki hii (Julai30-Agosti 3)

    (GMT+08:00) 2018-08-03 19:36:59

    Utoaji wa misaada ya kibinadamu kupitia Sudan kwenda Sudan Kusini kurefushwa kwa miezi sita

    Utoaji wa misaada ya kibinadamu kupitia Sudan kwenda Sudan Kusini sasa utarefushwa kwa miezi sita

    Kamishna anayeshughulikia misaada ya kibinadamu nchini Sudan Kusini Bw. Ahmed Adam, ametoa taarifa akisema Sudan na Sudan Kusini zimekubaliana kuendelea kupitisha misaada ya kibinadamu kwenye maeneo ya Sudan ili kuwafika wasudan kusini wenye mahitaji.

    Kwenye taarifa Bw Adam amesema utoaji misaada ya kibinadamu unaofanywa na Umoja wa mataifa kupitia Shirika la Mpango wa Chakula WFP, utaendelea, baada ya makubaliano kusainiwa na kurefusha muda wa utoaji wa msaada huo kwa miezi sita.

    Amesema mipango inaendelea kusafirisha tani elfu 65 za chakula kupitia njia mbalimbali ambazo Sudan imekubali kuzifungua. WFP pia inapanga kutuma tani elfu 30 za misaada ya kuokoa maisha, inayoweza kufika Sudan Kusini kwa njia ya ardhi kupitia miji ya Renk, Bentiu na Aweil.


    1  2  3  4  5  6  7  8  
    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako