• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Matukio makubwa yaliyotokea wiki hii (Julai30-Agosti 3)

    (GMT+08:00) 2018-08-03 19:36:59

    Idadi ya vifo kutokana na shambulizi la anga la Saudi Arabia nchini Yemen yaongezeka hadi 30

    Idadi ya waliofariki kutokana na shambulizi la anga lililofanywa na muungano wa kijeshi unaoongozwa na Saudi Arabia dhidi ya mji wa Al-Hudaydah wa Yemen, imeongezeka hadi 30 na raia wengine 50 wamejeruhiwa.

    Mpaka sasa muungano wa Saudi Arabia bado haujasema lolote kuhusu shambulizi hilo lililolenga bandari na soko la samaki, karibu na hospitali ya umma ya al-Thawra mjini humo.

    Mkurugenzi wa operesheni wa Ofisi ya uratibu wa mambo ya haki ya binadamu ya Umoja wa Mataifa OCHA Bw. John Ging amesema mapambano yanayopamba moto kwenye eneo la Hudaydah, yamefanya watu zaidi ya laki 3.4 kupoteza makazi yao tangu Juni 1.


    1  2  3  4  5  6  7  8  
    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako