• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Matukio makubwa yaliyotokea wiki hii (Julai30-Agosti 3)

    (GMT+08:00) 2018-08-03 19:36:59

    Watu 26 wauawa katika mashambulizi mawili Afghanistan

    Watu 18 wameuawa wakiwemo washambuliaji watatu na wengine 15 wamejeruhiwa katika shambulizi la kigaidi lililotokea jana dhidi ya jengo la ofisi ya serikali mjini Jalalabad, mashariki mwa Afghanistan, muda mfupi baada ya mkutano katika jengo hilo.

    Kati ya waliouawa kuna ofisa mmoja wa polisi na mwanamke mmoja, na majeruhi tisa wameondoka hospitali baada ya matibabu.

    Siku hiyohiyo, watu wanane waliuawa na wengine 40 walijeruhiwa baada ya basi walilokuwa wakisafiria kukanyaga bomu lililotegwa barabarani katika mkoa wa Farah, magharibi mwa Afghanistan, ambao umeshuhudia mapigano makali kati ya vikosi vya usalama na wapiganaji wa kundi la Taliban katika miezi kadhaa iliyopita.

    Hakuna kundi lolote lililotangaza kuwajibika na mashambulizi hayo.

    Wakati huo huo Gavana wa mkoa wa Jawzjan, kaskazini mwa Afghanistan Bw. Mawlawi Lutfullah Azizi amesema, wapiganaji 200 wa kundi la IS wakiwemo baadhi ya viongozi waandamizi wamesalimisha silaha zao katika wilaya ya Darzab mkoani humo.

    Hatua hiyo imekuja baada ya mapambano makali kati ya kundi la Taliban na kundi la IS kwenye wilaya hiyo na eneo jirani la Qush Tepa, ambapo katika wiki tatu zilizopita, wapiganaji 300 wa makundi hayo mawili waliuawa kwenye mapambano hayo.


    1  2  3  4  5  6  7  8  
    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako