• Idhaa ya Kiswahili
 • Uchumi
 • Michezo
 • Facebook
 • ChinaABC
 • Sayansi
 • Afya
 • Matukio makubwa yaliyotokea wiki hii (Septemba 1-Septemba 7)

  (GMT+08:00) 2018-09-07 18:54:59

  Jeshi la Somalia lawakamata wapiganaji 32 wa kundi la Al –Shabaab

  Jeshi la Somalia limewakamata wapiganaji 32 wa kundi la Al Shabaab wiki hii baada ya kufanya operesheni ya kijeshi katika mji wa Marka, wa eneo Lower Shabelle, kusini mwa Somalia.

  Kamanda wa jeshi la Somalia Bw. Odawa Yusuf, amesema katika operesheni hiyo iliyofanywa kwa muda wa siku mbili, baadhi ya wapiganaji walikamatwa wakiwa kwenye mapigano, wengine ni wapelelezi wa kundi hilo, wataalamu wa mabomu, na wakusanya kodi. Hatua hii imekuja siku chache baada ya jeshi la serikali kuutwaa mji huo kutoka kwa wapiganaji wa Al Shabaab.

  Habari nyingine zinasema wapiganaji wa Al Shabaab, wamewateka wazee 62 wa maeneo ya kati ya miji ya Guri'el, na Mataban, na kuwapeleka mjini Elbur, Galgadud.


  1  2  3  4  5  6  7  8  9  
  Webradio
  Sauti
  6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 1
  12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 2
  20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 3A
  • FM 3B
  Maoni yako