• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Matukio makubwa yaliyotokea wiki hii (Septemba 1-Septemba 7)

    (GMT+08:00) 2018-09-07 18:54:59

    Wanajeshi 10 Sudan Kusini wahukumiwa kwa kubaka

    Mahakama ya kijeshi nchini Sudan Kusini imewahukumu wanajeshi 10 vifungo vya kati ya miaka saba na maisha kutokana na ghasia ambapo mwandishi wa habari aliuawa na wafanyakazi wa kutoa huduma za kibinadamu kubakwa.

    Mahakama imeiamrisha serikali ya Sudan Kusini kumlipa kila muathiriwa wa ubakaji dola 4,000 kama fidia.

    Uhalifu huo ulitokea wakati wa shambulizi lililofanywa katika hoteli ya Terrain kwenye mji mkuu Juba mwaka 2016.

    Ripoti ya Umoja wa Mataifa iliwalaumu walinda amani kwa kushindwa kuitikia msaada wa waathiriwa.

    Wanajeshi wa Sudan Kusini wamelaumiwa kwa kuendesha uhalifu mara kadhaa tangu yazuke mapigano ya wenyewe kwa wenyewe mwaka 2013 lakini hili ndilo lilikuwa shambulizi baya zaidi dhidi ya raia wa kigeni.

    Hii ndiyo mara ya kwanza wanajeshi wameshukiwa kwa kuendesha uovu Sudan Kusini, taifa janga zaidi duniani ambalo lilipata uhusu wake mwaka 2011.


    1  2  3  4  5  6  7  8  9  
    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako