• Idhaa ya Kiswahili
 • Uchumi
 • Michezo
 • Facebook
 • ChinaABC
 • Sayansi
 • Afya
 • Matukio makubwa yaliyotokea wiki hii (Septemba 1-Septemba 7)

  (GMT+08:00) 2018-09-07 18:54:59

  Waziri mkuu wa Uingereza asema hakuna upigaji kura za maoni wa mara ya pili kuhusu Brexit

  Waziri Mkuu wa Uingereza Bi. Theresa May amekanusha habari kuwa kuna uwezekano wa kufanyika kwa mara ya pili kwa kura ya maoni ya mpango wa Uingereza kujitoa kwenye Umoja wa Ulaya Brexit, akisema kwamba hiyo itakuwa ni usaliti mkubwa dhidi ya demokrasia ya nchini Uingereza.

  Maoni yake hayo yamechapishwa jana usiku kwenye nakala ya mtandao ya gazeti la Daily Telegraph.

  Amesema serikali itatekeleza uamuzi wa kidemokrasia wa watu wa Uingereza kwa kuhakikisha nchi hiyo inajitoa rasmi kwenye Umoja wa Ulaya tarehe 29 ya mwezi machi mwaka 2019, na kwa kufanya hivyo anasema watajenga taifa lenye nguvu, na kuwa na mfumo wa serikali unaoongozwa na utaalamu na weledi zaidi, ambao utafaa kwa siku zijazo.

  Aliongeza kuwa serikali yake inaandaa mazingira mazuri kwa ajili ya Uingereza, na nchi hiyo sasa itaweza kudhibiti mipaka yake.

  Aidha, Bi. May amesisitiza kuwa kamwe hatashinikizwa kukubali maoni ambayo ni kinyume na matakwa ya taifa la Uingereza.


  1  2  3  4  5  6  7  8  9  
  Webradio
  Sauti
  6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 1
  12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 2
  20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 3A
  • FM 3B
  Maoni yako