• Idhaa ya Kiswahili
 • Uchumi
 • Michezo
 • Facebook
 • ChinaABC
 • Sayansi
 • Afya
 • Matukio makubwa yaliyotokea wiki hii (Septemba 30-Oktoba 5)

  (GMT+08:00) 2018-10-05 18:45:17
  Juhudi za kupambana na Ebola DRC zatatizwa na mapigano

  Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa linafanya ziara ya dharura kuelekea Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo kufuatia mapigano makali nchini humo ambayo yametatiza jitihada za kudhibiti kuzuka kwa virusi vya Ebola.

  Baraza hilo lenye wanachama 15 pia limeonya kuenea kwa Ebola kwa nchi za jirani na kuifanya kuwa vigumu zaidi kudhibiti.

  Ugonjwa huo umeua watu zaidi ya mia moja tangu Agosti 1.

  Mapigano makali kati ya makundi yaliyojihami katika mji wa Beni Mashariki mwa nchi yamewalynga pia wahudumu wa afya wa Umoja wa Mataifa na kupunguza kasi ya vita kuzuia kuenea kwa Ebola nchini DRC.

  Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Afya Duniani Dr Tedros Adhanom amesema kwamba wanachama wa baraza hilo wataelekea DRC Ijumaa ili kutathmini matatizo ambayo wahudumu wa Umoja wa Mataifa wanakabiliwa nayo katika kutoa msaada katika maeneo yaliyoathirika.

  Awali, alionya kwamba mapigano kati ya makundi yenye silaha katika eneo la Beni mashariki mwa nchi yaliwalazimu wafanyakazi wa afya kupunguza kasi ya matibabu ya wale walioathirika.

  Mpaka sasa, watu mia na sita wamekufa tangu mwanzo wa kuzuka kwaz homa hiyo mapema Agosti


  1  2  3  4  5  6  7  8  9  
  Webradio
  Sauti
  6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 1
  12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 2
  20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 3A
  • FM 3B
  Maoni yako