• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Matukio makubwa yaliyotokea wiki hii (Septemba 30-Oktoba 5)

    (GMT+08:00) 2018-10-05 18:45:17

    Zimbabwe kutoa chanjo ya kipindupindu kwa watu milioni 1.4

    Shirika la afya duniani WHO limesema Zimbabwe inazindua kampeni ya kutoa chanjo ya kipindupindu kwa watu milioni 1.4 ambao wako hatarini kupatwa ugonjwa huo, ikiwa ni sehemu ya jitihada zake za kudhibiti mlipuko wa ugonjwa huo.

    Kwa msaada wa WHO, Zimbabwe imetangaza hatua hiyo mjini Harare mwezi uliopita ambapo chanjo itatolewa kutoka kwenye hazina ya kimataifa inayofadhiliwa na Umoja wa chanjo duniani Gavi.

    Kampeni hiyo itakayotekelezwa kwa vipindi viwili itazingatia zaidi vitongoji vilivyoathirika vibaya zaidi huko Harare na Chitungwiza vilivyoko kilomita 30 Kusini Mashariki mwa mji mkuu wa nchi hiyo.

    Ili kuhakikisha kinga ya chanjo inafanya kazi kwa muda mrefu zaidi, dozi ya pili ya chanjo itatolewa katika maeneo yote wakati wa kipindi cha pili.


    1  2  3  4  5  6  7  8  9  
    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako