• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Matukio makubwa yaliyotokea wiki hii (Septemba 30-Oktoba 5)

    (GMT+08:00) 2018-10-05 18:45:17

    Watu zaidi ya elfu 70 wapoteza makazi kutokana na vurugu za kijamii magharibi mwa Ethiopia

    Ofisi ya uratibu wa misaada ya kibinadamu ya Umoja wa Mataifa UN-OCHA imesema watu zaidi ya elfu 70 wamepoteza makazi kutokana na vurugu za kijamii zilizotokea katika eneo la Kamashi jimboni Benishangul Gumuz, magharibi mwa Ethiopia.

    Ofisi hiyo imetoa taarifa ikisema kuwa vurugu hizo zilizoanzia wikiendi iliyopita zimesababisha watu zaidi ya elfu 70 kupoteza makazi yao au kukimbilia jimbo jirani la Oromia.

    Taarifa hiyo imeongeza kuwa vurugu hizo zilitokea baada ya maofisa waandamizi wanne kutoka jimbo la Benishangul Gumuz kuuawa Jumatano wiki iliyopita jimboni Oromia, wakati walipokuwa wakirudi nyumbani baada ya kushiriki mkutano wa usalama kati ya majimbo hayo mawili.

    Ofisa mkuu wa habari wa jimbo la Benishangul Gumuz Bw Zelalem Jaleta amesema kwamba vurugu hizo zimesababisha vifo vya watu wasiopungua 44, na wengine maelfu wamepoteza makazi yao.


    1  2  3  4  5  6  7  8  9  
    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako