• Idhaa ya Kiswahili
 • Uchumi
 • Michezo
 • Facebook
 • ChinaABC
 • Sayansi
 • Afya
 • Matukio makubwa yaliyotokea wiki hii (Septemba 30-Oktoba 5)

  (GMT+08:00) 2018-10-05 18:45:17

  Watu milioni 22.4 wakumbwa na msukosuko mkali wa chakula kwenye Pembe ya Afrika

  Shirika la uratibu wa misaada ya kibinadamu ya Umoja wa Mataifa UN-OCHA limesema wiki hiii kuwa watu milioni 22.4 kutoka nchi za Pembe ya Afrika wanahitaji msaada wa chakula.

  Katika taarifa yake kwa vyombo vya habari shirika hilo limetoa takwimu likisema watu laki 7 kutoka Kenya, milioni 1.6 wa Somalia, milioni 6.1 wa Sudan Kusini, milioni 7.9 wa Ethiopia na wengine milioni 6.2 kutoka Sudan wanakabiliwa na ukosefu wa chakula.

  OCHA imesema ingawa msaada wa kibinadamu na kunyesha kwa mvua nchini Somalia vimechangia kupunguza kidogo idadi ya watu wanaokumbwa na msukosuko wa chakula nchini humo, lakini mapambano na vurugu za kijamii zimepelekea ongezeko la idadi hiyo nchini Sudan na Sudan Kusini.

  Shirika hilo pia limeongeza kuwa nchi za Pembe ya Afrika pia zinakumbwa na msukosuko wa wakimbizi, kutokana na mapambano na vurugu za kijamii hususan katika nchi za Ethiopia, Somalia na Sudan Kusini.


  1  2  3  4  5  6  7  8  9  
  Webradio
  Sauti
  6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 1
  12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 2
  20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 3A
  • FM 3B
  Maoni yako