• Idhaa ya Kiswahili
 • Uchumi
 • Michezo
 • Facebook
 • ChinaABC
 • Sayansi
 • Afya
 • Matukio makubwa yaliyotokea wiki hii (Septemba 30-Oktoba 5)

  (GMT+08:00) 2018-10-05 18:45:17

  Rais wa Ghana arudi nyumbani kutoka Marekani baada ya kunusurika kwenye ajali ya ndege

  Rais Nana Akufo-Addo wa Ghana amerudi nyumbani baada ya kunusurika kwenye ajali ya ndege iliyotokea Jumamosi huko Washington, Marekani.

  Waziri wa habari mteule Bw. Kojo Nkrumah amethibitisha kuwa, moja ya injini za ndege ya rais Akufo-Addo wa Ghana ambayo iliwabeba rais na msafara wake, ambao walihudhuria kikao cha Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa ilizima takriban dakika 20 baada ya kuruka kutoka Washington.

  Duru zinasema ndege hiyo aina ya Falcon 900 iliruka kwa muda katika anga ya mji wa Washington ili kuchoma mafuta kabla ya kutua kwa msaada.

  Bw. Nkurumah amesema rais Akufo-Addo na msafara wake wamerudi nyumbani kwa ndege ya abiria ya Afrika Kusini.


  1  2  3  4  5  6  7  8  9  
  Webradio
  Sauti
  6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 1
  12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 2
  20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 3A
  • FM 3B
  Maoni yako