• Idhaa ya Kiswahili
 • Uchumi
 • Michezo
 • Facebook
 • ChinaABC
 • Sayansi
 • Afya
 • Matukio makubwa yaliyotokea wiki hii (Desemba 30-January 4)

  (GMT+08:00) 2019-01-04 19:32:06

  AMISOM yawaua wapiganaji 7 wa Al-Shabab kusini mwa Somalia

  Jeshi la Kenya limesema askari wake kwenye tume ya Umoja wa Afrika nchini Somalia AMISOM wamewaua magaidi saba wa kundi la Al-Shabab, na idadi isiyojulikana ya wapiganaji wa kundi hilo walikimbia wakiwa na majeraha kwenye eneo la kusini mwa Somalia.

  Msemaji wa jeshi la ulinzi la Kenya KDF Bw. Paul Njuguna amesema askari wawili wa Kenya walipata majeraha madogo kwenye mapambano yaliyotokea kwenye njia ya ugavi ya Tabda-Delahola, na kusisitiza kuwa askari wa Kenya wataendelea kuwasaka magaidi, ili kuhakikisha amani na usalama wa Kenya, na kuunga mkono operesheni za AMISOM kwa ajili ya kurejesha utulivu nchini Somalia.

  Habari nyingine zimesema wafanyakazi wawili wa Umoja wa mataifa na mkandarasi mmoja walijeruhiwa baada ya ofisi za Umoja wa mataifa mjini Mogadishu kushambuliwa kwa mizinga, na kundi la Al-Shabab limeripotiwa kutangaza kuwajibika na shambulizi hilo, ambalo ni la kwanza kutokea mwaka huu mpya.


  1  2  3  4  5  6  7  8  
  Webradio
  Sauti
  6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 1
  12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 2
  20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 3A
  • FM 3B
  Maoni yako