• Idhaa ya Kiswahili
 • Uchumi
 • Michezo
 • Facebook
 • ChinaABC
 • Sayansi
 • Afya
 • Matukio makubwa yaliyotokea wiki hii (Desemba 30-January 4)

  (GMT+08:00) 2019-01-04 19:32:06

  Ethiopia yawasamehe wafungwa zaidi ya 500 kwenye msimu wa Krismasi

  Serikali ya Ethiopia imetangaza kutoa msamaha kwa wafungwa 530 kwenye sherehe maalumu za sikukuu ya Krismasi ya kiethiopia.

  Shirika la utangazaji la Ethiopia Fana limesema wafungwa hao walipewa msamaha wakati Ethiopia inajiandaa kusherehekea sikukuu yake ya Krismasi Januari 7 kwa ajili ya kukumbuka kuzaliwa kwa Yesu Kristo kutokana na mila za kanisa la ki-orthodox la Ethiopia.

  Kwa mujibu wa ofisi ya mwanasheria mkuu, msamaha huo umetolewa ikiwa ni sehemu ya mchakato unaoendelea wa maafikiano ya kitaifa.

  Kabla ya hapo, Ethiopia ilitoa msamaha kwa maelfu ya wafungwa wakati iliposherehekea sikukuu ya mwaka mpya Septemba 11 mwaka jana.


  1  2  3  4  5  6  7  8  
  Webradio
  Sauti
  6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 1
  12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 2
  20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 3A
  • FM 3B
  Maoni yako