• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Matukio makubwa yaliyotokea wiki hii (Desemba 30-January 4)

    (GMT+08:00) 2019-01-04 19:32:06

    Bunge jipya la Marekani laanza vikao likiwa limegawanyika

    Bunge la Marekani limanza vikao vyake wiki hii huku chama cha Democrat kikiwa na wingi wa wabunge 235 dhidi ya 199 wa chama cha Republican. Kiti kimoja cha bunge bado kina migogoro kutokana na tuhuma za udanganyifu kwenye uchaguzi. Bibi Nancy Pelosi amechaguliwa kuwa spika wa baraza la chini la bunge.

    Bibi Pelosi amechaguliwa mara ya pili kuwa spika, na kuwa mwanamke pekee katika historia ya Marekani kushika nafasi hiyo.

    Makamu wa Rais wa Marekani Bw. Mike Pence ambaye ni mwenyekiti wa baraza la seneti amewaapisha maseneta wapya, na sasa chama cha Republican kina wingi wa wajumbe 53 dhidi ya 45 wa chama cha Democrat, na maseneta wawili wa kujitegemea wanaounga mkono upande wa Democrat.


    1  2  3  4  5  6  7  8  
    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako