• Idhaa ya Kiswahili
 • Uchumi
 • Michezo
 • Facebook
 • ChinaABC
 • Sayansi
 • Afya
 • Matukio makubwa yaliyotokea wiki hii (Desemba 30-January 4)

  (GMT+08:00) 2019-01-04 19:32:06

  Kiongozi wa Korea Kaskazini asema ataendelea na mpango wa kuondoa silaha za nyuklia

  Kiongozi wa Korea Kaskazini Bw. Kim Jong Un amesogeza mbele mpango wake wa nyuklia na majaribio yake ya makombora kwenye Peninsula na kukubali kukutana na rais Donald Trump wa Marekani muda wowote.

  Katika salamu zake za mwaka mpya zilizorushwa na televisheni ya taifa nchini humo, kiongozi huyo wa Korea Kaskazini amesisitiza uamuzi wake wa kufanya kazi ya kujenga uhusiano mpya na Marekani, kuanzisha amani ya kudumu kwenye Peninsula ya Korea.

  Amebainisha kuwa yupo tayari kufungua tena eneo la kiwanda kati ya Korea Kaskazini na Korea Kusini katika mji wa Kaesong na kuendelea na mpango wa utalii katika mlima Kumgang pwani ya mashariki bila ya sharti lolote.

  Wakati huo huo Rais Donald Trump wa Marekani amesema, anatarajia kufanya mkutano wa pili na kiongozi wa Korea Kaskazini Bw. Kim Jong Un katika siku za baadaye. Rais Trump amewaambia wanahabari kwenye ikulu ya Marekani kuwa amepata ujumbe mzuri kutoka Bw. Kim.

  Rais huyo wa Marekani alidokeza mapema mwezi Desemba kuwa mkutano wa pili kati yake na Bw. Kim utaweza kufanyika mwezi Januari au Februari, ameongeza kuwa wataweza kufanya mkutano mwingine unaopangwa kufanywa katika siku za baadaye.


  1  2  3  4  5  6  7  8  
  Webradio
  Sauti
  6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 1
  12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 2
  20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 3A
  • FM 3B
  Maoni yako