• Idhaa ya Kiswahili
 • Uchumi
 • Michezo
 • Facebook
 • ChinaABC
 • Sayansi
 • Afya
 • Matukio makubwa yaliyotokea wiki hii (Desemba 30-January 4)

  (GMT+08:00) 2019-01-04 19:32:06

  Sudan yatarajia kupunguza mfumuko wa bei hadi kufikia asilimia 27.1 mwaka 2019

  Benki kuu ya Sudan imesema inalenga kupunguza mfumuko wa bei hadi kufikia asilimia 27.1 katika mwaka huu.

  Akiongea na wanahabari mjini Khartoum mkuu wa benki kuu ya Sudan Bw. Mohamed Khair al-Zubair amesema sera za benki hiyo kwa mwaka huu zinalenga kutimiza utulivu wa kifedha, ili kuhakikisha ukuaji endelevu wa uchumi unafikia asilimia 5.1.

  Kwa mujibu wa ofisa huyo, sera za benki hiyo kwa mwaka huu ni pamoja na kupunguza mfumuko wa bei, kutuliza kiwango cha ubadilishaji wa fedha, kuimarisha imani ya watu kwa mfumo wa benki na kuongeza rasilimali za fedha za kigeni kwa ajili ya kutimiza utulivu wa kifedha.

  Imefahamika kuwa kiwango cha mfumuko wa bei nchini Sudan kiliongezeka na kufikia hadi asilimia 68.93 mwezi Disemba mwaka 2018, kutoka asilimia 25.15 ya mwezi Disemba mwaka 2017.

  Sudan imeshuhudia msukosuko mkubwa wa kiuchumi tangu itengane na Sudan Kusini mwaka 2011, ambako kumepunguza asilimia 75 ya mapato yaliyotokana na biashara ya mafuta.


  1  2  3  4  5  6  7  8  
  Webradio
  Sauti
  6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 1
  12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 2
  20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 3A
  • FM 3B
  Maoni yako