• Idhaa ya Kiswahili
 • Uchumi
 • Michezo
 • Facebook
 • ChinaABC
 • Sayansi
 • Afya
 • Matukio makubwa yaliyotokea wiki hii (February 16-February 22)

  (GMT+08:00) 2019-02-22 18:59:17

  Museveni kuwania urais mwaka 2021.

  Chama tawala nchini Uganda kimemteua Rais Yoweri Kaguta Museveni kuwa mgombea wake wa urais katika uchaguzi wa mwaka 2021.

  Hii inamaana ya kuwa, kiongozi huyo mwenye miaka 74, na aliyeingia madarakani mwaka 1986, atagombea urais kwa muhula wa sita.

  Chama cha National Resistance Movement (NRM) kimekubali, katika kikao kilichoongozwa na Museveni jana Jumatano kuwa Museveni aendelee kuongoza harakati na taifa mwaka 2021 na kuendelea ili kuondosha vikwazo vya mabadiliko na maendeleo.

  Miaka ya nyuma, Museveni aliwahi kusema kuwa, viongozi wanaodumu madarakani ndio chanzo cha matatizo barani Afrika.

  Hata hivyo, wakati akigombea muhula wa tano wa madaraka mwaka 2016, alisema kuwa huo haukuwa muda muafaka kwake kuondoka madarakani kwani bado alikuwa na kazi ya kufanya.

  Ugombea wake katika uchaguzi ujao unakuja baada ya kusaini kuwa sheria mswada ambao uliondoa ukomo wa urais wa miaka 75.

  Hata hivyo, kupitishwa kwa muswada huo bungeni kuligubikwa na vurumai kubwa kutokana na kupingwa na wabunge wa upizani.

  Mahakama ya Upeo ya Uganda mwezi wa Januari imeanza kusikiliza shauri la kupinga mabadiliko hayo ya sheria.


  1  2  3  4  5  6  7  8  
  Webradio
  Sauti
  6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 1
  12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 2
  20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 3A
  • FM 3B
  Maoni yako