• Idhaa ya Kiswahili
 • Uchumi
 • Michezo
 • Facebook
 • ChinaABC
 • Sayansi
 • Afya
 • Matukio makubwa yaliyotokea wiki hii (February 16-February 22)

  (GMT+08:00) 2019-02-22 18:59:17
   

  Wabunge saba wajiuzulu Uingereza

  Wabunge saba kutoka chama kikuu cha upinzani nchini Uingereza cha Labour ambao hawakubaliani na kiongozi wao Jeremy Corbyn kuhusu Uingereza kujitoa katika Umoja wa Ulaya na vita dhidi ya ubaguzi, wamejiuzulu Jumatatu wiki hii.

  Miongoni mwa wabunge waliojiuzulu ambao wanadai kuwa wanaunda "kundi lisiloegemea" ni pamoja na Chuka Umunna, ambaye ameonekana kuwa mpinzani na uongozi wa chama cha Labour na Luciana Berger, ambaye anakosoa mwenendo wa chama chake kwa vita dhidi ya ubaguzi. Hata hivyo Jeremy Corbyn amesema anasikitishwa na uamuzi wa wabunge hao.

  Kundi hili la wabunge saba lilikuwa likimuitisha, wiki moja sasa, kubadili kuhusu mkakati na kufanya kampeni kwa kura ya pili ya maoni kuhusu kujiunga na Umoja wa Ulaya.

  Kujiuzulu kwa wabunge hawa kunaweza kusababisha mgawanyiko mkubwa katika chama hiki cha Labour, kwa mujibu wa chanzo kilio karibu na chama cha Labour.


  1  2  3  4  5  6  7  8  
  Webradio
  Sauti
  6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 1
  12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 2
  20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 3A
  • FM 3B
  Maoni yako