• Idhaa ya Kiswahili
 • Uchumi
 • Michezo
 • Facebook
 • ChinaABC
 • Sayansi
 • Afya
 • Matukio makubwa yaliyotokea wiki hii (March 16-March 22)

  (GMT+08:00) 2019-03-22 20:05:10

  Brenton Tarrant, raia wa Australia aliyeshtakiwa kwa mauaji, alipata leseni ya kumiliki silaha nchini New Zealand mnamo 2017.

  Brexit kuahirishwa hadi Mei 22 ikiwa mpango wa uahirishaji utapitishwa na wabunge wa Uingereza

  Mpango wa Uingereza kuondoka rasmi kutoka kwa Umoja wa Ulaya umeahirishwa hadi Mei 22 ikiwa mpango wa uahirishaji utapitishwa na wabunge wa Uingereza

  Mwenyekiti wa Baraza la Ulaya Bw. Donald Tusk amesema, nchi 27 wanachama wa Umoja huo zimeafiki kwa kauli moja kurefusha utekelezaji wa kifungu cha 50 hadi Mei 22, ikiwa Makubaliano ya kujitoa Umoja wa Ulaya Brexit yataidhinishwa na Baraza la Makabwela la Bunge la Uingereza wiki ijayo.

  Bw. Tusk ameongeza kuwa, endapo Makubaliano ya Brexit hayatapitishwa wiki ijayo, tarehe ya Brexit itaahirishwa hadi Aprili 12.

  Nchi 27 wanachama wa Umoja wa Ulaya pia zilipitisha Makubaliano ya Strasbourg na kuendelea kufanya maandalizi ya Brexit isiyo na makubaliano.


  1  2  3  4  5  6  7  
  Webradio
  Sauti
  6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 1
  12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 2
  20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 3A
  • FM 3B
  Maoni yako