• Idhaa ya Kiswahili
 • Uchumi
 • Michezo
 • Facebook
 • ChinaABC
 • Sayansi
 • Afya
 • Matukio makubwa yaliyotokea wiki hii (March 16-March 22)

  (GMT+08:00) 2019-03-22 20:05:10

  Kampuni ya Boeing yarejea ahadi yake ya usalama wa ndege kufuatia ajali ya ndege ya Ethiopia

  Mkurugenzi mtendaji wa Kampuni ya Boeing Bw. Dennis Muilenburg amesema kampuni yake itaendelea kushikilia msingi wake wa kuthamini usalama ambao imesimamia katika biashara ya safari za anga kwa zaidi ya miaka 100.

  Katika barua ya wazi iliyotolewa mwanzoni mwa wiki hii kwa mashirika ya ndege, abiria na jamii ya safari za anga, Bw. Muilenburg amezungumzia kuongezeka kwa wasiwasi kuhusu usalama wa ndege za kampuni hiyo kutokana na ajali mbaya ya ndege ya Shirika la Ndege la Ethiopia namba 302 iliyoanguka na kusababisha vifo vya abiria 157 pamoja na wahudumu.

  Ajali hiyo ni ya pili inayohusisha ndege aina ya Boeing 737 MAX 8, baada ya ndege ya Indonesia Lion Air kuanguka mwezi Oktoba nchini Indonesia na kusababisha vifo vya watu 189.

  Ripoti iliyotolewa na taasisi ya uchunguzi wa usalama wa ndege ya nchini Ufaransa imesema, chanzo cha ajali ya ndege ya Boeing ya kampuni ya ndege ya Ethiopia kinafanana na ajali ya ndege ya Boeing ya kampuni ya ndege ya Lion ya Indonesia.

  Ripoti hiyo imesema, idara ya uchunguzi wa ajali ya Ethiopia, kamati ya usalama wa usafiri ya Marekani na taasisi hiyo vitathibitisha chanzo hicho kwa kutumia visanduku vyeusi viwili.


  1  2  3  4  5  6  7  
  Webradio
  Sauti
  6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 1
  12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 2
  20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 3A
  • FM 3B
  Maoni yako